Monday, 27 February 2017

TECNO L9 NA L9 PLUS NI TOLEO LIJALO KWA SIMU ZA TECNO


Tetesi ni kwamba Tecno wanategemea kuleta wanafamilia wengine kwenye series ya L ambao si wengine ni L9 na L9 plus , kwa tetesi ni kwamba zinakaribia kuzinduliwa hivi karibuni.
Simu za tecno katika familia ya L Series zina aminika kwa utunzaji wake wa betri kwakuwa zinawekewa betri zenye nguvu kubwa kama tuliovyoona kwenye L8 na L8 plus zilozo kuwa na betri zenye nguvu ya 5050 mAh. Kwa hiyo tutegeme vivyo hivyo kwenye tecno L9 na L9 plus.

Sifa nyinginezo za kutegemea ni muundo bora kabisa pamoja na mabadiliko katika software , pia kwa upande wa  RAM L9 inategemewa kuwa na 2GB wakati L9 plus ni 3GB RAM.
Pia simu hizo zinatarajiwa kuja pamoja na Android version ya sasa ya 7.0 nougat.

Kuwa karibu na blogu hii kupata sifa zote za simu hizo pindi tu zitapo toka.

No comments:

Post a Comment